1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya kandanda la kuwania kombe la ulaya imeanza Uswisi

7 Juni 2008

-

Fainali za 13 za kandanda kuwania kombe la Ulaya zimeanza leo huko Uswisi kwa pambano kati ya wenyeji Uswisi na Jamuhuri ya Czech.

Timu 16 zinashiriki katika fainali hizo ambazo mwaka huu zinaandaliwa kwa pamoja kati ya Uswis na Austria.

Mechi nyingine katika siku hii ya kwanza ya ufunguzi ni kati ya Ureno na Ugiriki.

Ujerumani mabingwa mara tatu wa kombe hilo, wanaanza kampeni za kuwania kombe hilo kesho kwa kupambana na Poland huko Austria.

Idhaa ya kiswahili ya DW itakuwa ikikuletea taarifa zote kuhusu michuano hiyo.