1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tujifunze Mashariki ya Kati kukabili halijoto ulimwenguni

Hawa Bihoga
5 Juni 2023

Kadri joto linavyozidi kuongezeka, Mashariki ya Kati itashuhudia ongezeko la vifo vitokanavyo na joto kali. Licha ya mapungufu ya mipango wataalamu wanadokeza kwamba eneo hilo linaweza kupigiwa mfano kuhusu joto kali.

Klima Hitzewelle l Spanien, Andalusien Seville
Picha: Cristina Quicler/AFP

Mwanzilishi wa mtandao wa waandishi wa habari wanawake mjini Baghdad wanaoandikia masuala ya hali ya hewa, Kholoud al-Amiry, ameiambia DW kwamba wakati hali ya joto inapotishia kupanda juu ya kiwango kinachotumika wakati wa kuoka kwa nyuzi joto 50 katika kipimo cha Celsius nchini Iraq, kwa kawaida wakaazi wanapata likizo na kuhimizwa kusalia majumbani.

Anasema watu hujifunza kuishi na hali hiyona wanabadilika kadri hali inavyokwenda, marekebisho hayo yanajumuisha pia kila kitu ikiwemo hata kurekebisha makaazi yao.

Soma pia:Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya ongezeko la joto

Mnamo mwezi Mei, utafiti mpya ulichapishwa katika jarida la sayansi la Nature Sustainability, likiainisha athari za joto kali duniani kote, hali ya joto kimataifa itapanda kwa zaidi ya nyuzi joto 2.7 katika kipimo cha Celsius katika kipindi cha miaka 50 ijayo.

Tafiti zataka kuchukuliwe hatua madhubuti

Mnamo mwezi Aprili, utafiti mwingine uliochapishwa katika jarida la matibabu la Uingereza The Lancet uliangalia jinsi vifo vingi zaidi vinavyohusiana na joto vinaweza kutokea katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ikiwa sayari itaendelea kuwa na joto.

Watu wakijipoza na joto kwenye moja ya ufukwe MarekaniPicha: Ringo H.W. Chiu/AP/picture alliance

Utafiti unasema idadi ya wenyeji katika eneo hilo ambao watakufa kutokana na sababu zinazohusiana na joto kila mwaka inaweza kuongezeka kutoka wastani wa vifo viwili kati ya watu 100,000 hivi sasa hadi 123 kwa kila watu 100,000 katika miongo miwili iliyopita kwa karne hii.

Soma pia:Kiwango cha joto duniani kuongezeka kwa nyuzi 1.5 katika miaka 5 ijayo

Utafiti wa Lancet pia ulibainisha kuwa idadi ya watu na ongezeko la watu kuingia katika miji ya Mashariki ya Kati itakuwa na athari juu ya jinsi joto kali linavyoathiri wenyeji.

Kufikia miaka ya 2050, karibu 70% ya watu wanatarajiwa kuishi katika miji mikubwa na kufikia 2100, wazee watakuwa wengi kuliko vijana katika eneo hilo.

"Uzee na msongamano mkubwa wa watu ni sababu kuu za hatari kwa magonjwa yanayohusiana na joto na vifo," waliandika watafiti kutoka chuo cha London of Hygiene & Tropical Medicine pamoja Taasisi ya Cyprus.

Mipango itawasaidia wananchi wa kawaida

Mipango ya hatua za kukabiliana na joto huwasaidia wananchi wa kawaida kukabiliana na joto kali. Zinaweza kujumuisha kila sekta kuanzia kujengwa kwa "vituo vya kupoza" vinavyoendeshwa na serikali.

Maeneo ya umma ambapo watu wanaweza kwendakujikinga na joto na kunywa maji ambapo hatua za maandalizi, kama vile kampeni za uelimishaji kuhusu jinsi ya kuhifadhi baridi wakati wa joto kali au kupanda miti zaidi katika miji.

Je Unajua namna hali ya hewa inavyoathiri afya yako?

03:16

This browser does not support the video element.

Hata hivyo, nchi nyingi za Ulaya tayari zina mipango kama hii ikiwemo na mchakato wa kuendeleza, lakini mataifa mengi ya Mashariki ya Kati hayafanyi hivyo, licha ya hatari inayoongezeka kwa kasi.

Ingawa nchi nyingi za Mashariki ya Kati zimepitisha sheria juu ya maendeleo endelevu na ulinzi wa mazingira, nyingi "bado hazina maono ya wazi kuhusu jinsi ya kushughulikia athari za muda mrefu za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya ya umma," wataalam wa afya ya umma wanahoji.

Soma pia:Vifo 1,200 kwa mwaka barani Ulaya kutokana na Uchafuzi wa hali ya hewa

Mfano mwingine unatoka Yemen, ambako kumekuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2014, kuwa na uwezo wa kutabiri matukio ya joto kali ni sehemu kubwa ya mipangoya hatua ya joto inayofadhiliwa na serikali.

Sylvia Bergh, profesa wa usimamizi wa maendeleo na utawala katika Chuo Kikuu cha Erasmus Rotterdam, aliiambia DW, kuwa licha ya hayo watu wanaoishi katika eneo hilo wamezoea viwango vya juu vya joto na tayari wanaelekea kuishi katika nyumba zenye baridi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW