1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Miezi mitano ya mradi wa treni ya kisasa Tanzania

Deo Kaji Makomba
23 Januari 2025

Shughuli za usafirishaji abiria katika treni ya mwendo kasi ya umeme ya SGR kutoka jiji la kibiashara Dar es Salaam hadi Dodoma makao makuu ya Tanzania imerahisisha usafiri licha ya changamoto kadhaa.

Treni ya umeme ya Tanzania
Mradi wa treni ya kisasa ya umeme - SGR uliigharimu serikali ya Tanzania dola bilioni 80Picha: Tanzania State House

Huko nchini Tanzania ikiwa takribani miezi mitano imepita tangu kuanza kwa shughuli za usafirishaji abiria katika treni ya mwendo kasi ya umeme ya SGR kutoka jiji la kibiashara Dar es salaam hadi Dodoma makao makuu ya Tanzania imerahisisha usafiri licha ya changamoto kadha wa kadha zinazokabili treni hiyo ya kisasa ambayo ni ya kwanza katika eneo la ukanda wa Afrika Mashariki. 

Mnamo Juni 14 mwaka 2024 nchi Tanzania iliandika historia kwa kuanza safari ya SGR kati ya Dar es salaam na Morogoro baada ya majaribio kadhaa yakiwemo ya Februari 27 mwaka 2024. Agosti Mosi mwaka 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alizindua safari kati ya Dar es salaam hadi Dodoma.

Mnamo Juni 14 mwaka 2024 nchi Tanzania iliandika historia kwa kuanza safari ya SGR kati ya Dar es salaam na MorogoroPicha: Florence Majani/DW

Akizungumza na DW katika kituo kikuu cha treni ya SGR jijini Dodoma, mkurugenzi mkuu mtendaji wa Shirika la Reli nchini Tanzania, Bwana Masanja Kadogosa anasema kuwa mradi huo wa treni ya umeme ya mwendo kasi umekuwa msaada mkubwa kwa usafiri wa abiria licha ya changamoto ndogo ndogo za hapa na pale.

Bwana Kadogosa ameongeza kusema kuwa tangu kuanza kwa safari za abiria kutoka Dar es salaam, Morogoro hadi Dodoma makao makuu ya Tanzania, kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana ikiwemo kufanya safari kuwa fupi ukilinganisha na usafiri wa treni ya zamani na kwamba hadi hivi sasa zaidi ya abiria milioni moja na laki tano wametumia usafiri huo.

Safari ya majaribio ya treni ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma

01:30

This browser does not support the video element.

Lakini licha ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa safari za treni hiyo ya SGR, zipo changamoto zinazokabili mradi huo kama navyoeleza Masanja Kadogosa, Mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la reli nchini Tanzania.

Tangu kuanza kwa safari za treni ya mwendo kasi ya umeme ya SGR, kumepokelewa kwa maoni mseto. Abraham Mtongore Bayo na Agnes Sanga ni miongoni mwa abiria ambao wamekuwa wakitumia usafiri huo.

Kwa upande wake serikali ya Tanzania kupitia msemaji mkuu wake Greson Msigwa, anasema kuwa wananchi wanapaswa kutunza miundo mbinu ya mradi huo na kwamba hatua kali zimekuwa zikichukuliwa kwa wale wote wanaojihusisha na uhujumu wa mradi huo wa kimkakati.

Ujenzi wa mradi huo katika vipande vilivyosalia kutoka Makutupora Dodoma kwenda Tabora hadi Mwanza unaendelea huku mamlaka husika zikileza kuwa mradi huo unatarajia kukamilika mnamo mwaka 2028.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW