1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miezi mitatu toka mji wa Bukavu udhibitiwe wa waasi wa M23

Idhaa ya kiswahili16 Mei 2025

Hadi sasa, bado wakazi wa mji huo wanazidi kushuhudia baadhi ya masaibu wanayopitia licha yakuwa viongozi wa AFC/M23 wanatathmini mabadiliko chanya.

Wapiganaji wa AFC/M23 wanadhibiti mji wa kimkakati wa Bukavu, ambao wameumiliki kwa miezi mitatu
Wapiganaji wa AFC/M23 wanadhibiti mji wa kimkakati wa Bukavu, ambao wameumiliki kwa miezi mitatuPicha: Ernest Muhero/DW

Wakazi wengi wa Bukavu wanasema kinachowaathiri ni hasa hali ya ukosefu wa usalama inayoendelea lakini pia matatizo mengi ya kiuchumi.

Mbali na mauaji yanayoendelea, visa vya watu kujilipishia kisasi na magereza yaliyo bomolewa mjini Bukavu napia katika vijiji ambavyo viko chini ya AFC/M23, wakazi wanalazimishwa kulipa ushuru mwengi hasa kwa magari yanayotembea kwenye barabara zinazopeleka vijijini, wakati huu ambapo wengi wao wanakumbwa na matatizo yakiuchumi.

Lakini pia, wakaazi wengi wanalaani vizuizi vya kisiasa wakisema kwasasa hawana uhuru wa maoni au wa maandamano. Wengi pia wanasema wanakumbuka vipindi vya kisiasa ambayo vimepigwa marufuku kwenye vyombo vya habari.

Na katika baadhi ya vijiji kama vile Kamanyola, shughuli za asasi za kiraia zimepigwa marufuku na mamlaka mpya ya AFC/M23.

Hili ndilo linalomsikitisha mwanaharakatii huyu wakisiasa ambaye ambaye hakutaka jina lake litajwe, na anayependelea kukaa kimya nyumbani kwake ili aepuke matatizo.

Changamoto sio tu za kiusalama lakini pia za kiafya

Raia wa Goma na Bukavu wanatumai kupata amani ya kudumu na suluhisho la kisiasa kwa vitaPicha: Ernest Muhero/DW

Pia, wanaharakati wa masuala ya afya wanatoa malalamiko kuhusu kuzorota kwa hali ya afya katika vijiji kadhaa ambapo miundo ya afya haipewi tena dawa na pembejeo nyingine za afya. Wanasema matokeo yake nikwamba mlipuko wa magonjwa kama vile M-Pox, surua, kipindupindu na malaria unaendelea.

Miezi mitatu baada ya kutekwa kwa Bukavu, mji huo hauna polisi wakulinda usalama katika vitongoji na barabarani. Hata hivyo, meya wa Bukavu chini ya AFC/M23 Ladis Muganza anahakikishia kuwa hali inazidi kuimarika.

Licha ya hayo, matumaini ya wakongo bado yapo kwenye mazungumzo kati ya serikali ya Kongo na AFC/M23 mjini Doha nchini Qatar,  na pia wanatarajia kusainiwa kwa mkataba wa amani kati ya nchi yao na Rwanda chini ya usaidizi wa Marekani ili amani irejee Mashariki mwa Kongo, hata kama wakazi wengine kwasasa wameanza kutilia shaka kinachoendelea na kujiuliza maswali.