1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mifumo ya satelaiti ya shirika la utangazaji Iran yadukuliwa

19 Januari 2026

Wadukuzi walivuruga mifumo ya upeperushaji wa matangazo ya televisheni ya taifa ya Iran kwa njia satelaiti na kupeperusha video zinazomuunga mkono mwanamfalme wa nchi hiyo Reza Pahlavi aliye uhamishoni.

Marekani Washington D.C. 2026 | Reza Pahlavi wakati wa mkutano na waandishi wa habari
Mwanamfalme wa Iran aliye uhamishoni, Reza Pahlavi Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Kanda hiyo ilipeperushwa usiku wa jana katika vituo vingi vinavyorusha matangazo yao kwa kutumia satelaiti ya shirika la utangazaji la Jamhuri hiyo ya Kiislamu ya Iran, lililodhibiti  utangazaji wa televisheni na redio.

Video hiyo ilimuonyesha Pahlavi, kisha ikajumuisha kanda ya vikosi vya usalama na wengine walioonekana kuvaa sare za polisi wa Iran.

Ilidai bila kutoa ushahidi kuwa maafisa wengine wa usalama "wameweka silaha zao chini na kula kiapo cha utii kwa watu."Udukuzi huo unakuja huku idadi ya vifo vilivyotokana na maandamano nchini humo ikifikia takriban watu 3,919. Haya ni kwa mujibu wa wanaharakati nchini Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW