1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mifumo ya ulinzi ya Urusi yadungua droni 54 za Ukraine

18 Septemba 2024

Jeshi la anga la Urusi limetangaza kuharibu droni 54 zinazodaiwa kurushwa na Ukraine usiku kucha zikilenga maeneo matano ya Urusi.

Mfumo wa ulinzi wa anga
Mfumo wa ulinzi wa angaPicha: SERGEI SUPINSKY/AFP/Getty Images

Jeshi la anga la Urusi limetangaza kuharibu droni 54 zinazodaiwa kurushwa na Ukraine usiku kucha zikilenga maeneo matano ya Urusi, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la nchi  hiyo TASS lililoinukuu wizara ya Ulinzi nchini humo. 

Nusu ya droni hizo zilidunguliwa katika anga ya eneo la mpakani la Kursk huku nyengine zikiangushwa katika maeneo ya Bryansk, Smolensk, Oryol na Belgorod. 

Soma pia: Rais Volodymyr Zelensky asema jeshi lake limepungukiwa silaha katikati ya uhitaji

Hata hivyo, shirika hilo la habari la TASS halikulitaja eneo la Tver ambako maafisa wamesema shambulizi la droni lilisababisha moto mkubwa na kulazimisha watu walioko karibu na mji wa Toropets kuhamishwa na kupelekwa katika maeneo salama.