Migogoro na majanga vimeacha watu milioni 76 bila makazi
14 Mei 2024Matangazo
Vita katika nchi za Sudan Kongo na Mashariki ya Kati vimesababisha thuluthi mbili ya watu kuhama kwa mujibu wa shirika kubwa linalofuatilia masuala ya uhamiaji duniani. Ripoti ya shirika hilo imebaini kwamba idadi ya wakimbizi wa ndani imefikia asilimia 50 katika kipindi cha miaka 5 iliyopita na imeongezeka mara mbili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Ripoti hiyo imechapishwa kutokana na utafiti uliofuatilia nyendo za watu milioni 46.9 katika mwaka 2023 baada yamatukio ya majanga ya asili kama mafuriko.Kiasi ya watu milioni 75.9 wanaishi katika mazingira ya kuwa wakimbizi wa ndani katika mataifa yao kufikia mwishoni mwa mwaka jana na wengi wako katika mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara,barani Afrika.