Migomo nchini Afrika Kusini yaendelea kwa siku ya tatu
29 Julai 2009Matangazo
Wakaazi wa maeneo ya madongo poromoka katika majimbo kadhaa waliandamana kutaka huduma bora kwa umma, huku wafanya kazi wa manispaa wakiandamana pia kwa siku ya tatu leo wakishikilia waongezewe mishahara. Wakati huo huo, wafanya kazi katika sekta ya viwanda vya kemikali wametangaza kuumaliza mgomo wao wa siku nane baada ya kupewa nyongeza ya mishahara baina ya asilimia tisa na kumi. Uchumi wa Afrika Kusini unajionea kwenda chini sana kuwahi kuonekana tangu mwaka 1992, na vyama vya wafanya kazi vinasema hali hiyo inawaumiza sana walio maskini. Othman Miraji alimuuliza kwa njia ya simu mwandishi wa habari Issac Khomu juu ya mgomo wa wafanyakazi wa manispaa, unaendelea vipi? Mwandishi: Othman Miraji Mhariri: Mohamed Abdulrahman