1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mihadarati na vileo - Poromoko la jamii

5 Septemba 2012

Idadi ya watumiaji wa madawa ya kulevya barani Afrika imepanda kwa kiwango cha kuogopesha katika miaka iliyopita. Mfululizo wa vipindi hivi unatuonyesha jinsi ilivyo rahisi kuingia katika utumiaji wa madawa ya kulevya.

Learning by Ear – Drugs and substance abuse Fotograf | Bildagentur: © Kuni Takahashi, Polaris, LAIF | (Mann mit Zigarette) ACHTUNG!! DIE DEUTSCHE WELLE HAT DIE NUTZUNGSRECHTE NUR BIS 1.9.2013!! EINSTELLUNGSDATUM: 09.09.2011
Picha: LAIF

Madawa ya kulevya si jambo geni katika jamii ya Kiafrika. Madawa aina ya Khat yanayopatikana Afrika ya Mashariki tayari yameshakuwa sehemu ya utamaduni na nchini South Afrika pia utumiaji wa Cannabis ni sehemu ya utamaduni wa jamii. Lakini kutokana na kuongezeka kwa umaskini, kuharibika kwa mfumo wa kijamii , uhamiaji wa wafanyakazi pamoja na uhamiaji kutoka sehemu za vijijini, utumiaji wa madawa ya kulevya unashindwa kuzuilika. Madawa makali ya kulevya hutumika zaidi hasa katika maeneo ya mabanda kwenye majiji makubwa. Pia utumiaji wa sigara pamoja na pombe umeongezeka kutokana na usambazaji kurahisishwa na kwa sababu ya matangazo mengi yanayofanywa kwa ajili ya bidhaa hizo.

Athari zinazotokea katika jamii ni za hatari sana. Mchezo wetu wa redio wa kusisimua unaonyesha hilo kwa kutumia mfano wa Jabali, Zula na Okosho, vijana wanaokumbana na utumiaji wa madawa ya kulevya na kujifunza athari zake zenye maumivu. Lakini masimulizi yetu yataangazia mbali zaidi ya marafiki wetu watatu kwani hata viongozi wakubwa wa serikali wanahusika katika kashfa ya uuzaji wa madawa ya kulevya.

Vipindi vya Deutsche Welle “Learning by Ear – Noa Bongo! Jenga Maisha Yako” vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharic.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW