Miili 10 zaidi ya waliokufa kwa njaa Kenya yafukuliwa
25 Aprili 2023Matangazo
Kwa siku kadhaa polisi wamekuwa wakifanya uchunguzi katika msitu wa Shakahola karibu na mji wa pwani wa Malindi, baada ya kupewa taarifa kuhusu madhehebu ya itikadi kali ya mhubiri Paul Mackenzie Nthenge, aliyewahimiza wafuasi wake kufunga hadi kufa ili kukutana na Mungu. Miili 10 iliyofukuliwa leo ilijumuisha watoto watatu, wakati pia waokozi waliwapata manusura wawili waliodhoofika kabisa. Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki anatarajiwa kuzuru eneo hilo hii leo, huku Rais William Ruto akiapa kuchukua hatua dhidi ya wahubiri bandia wanaotaka kutumia dini ili kueneza itikadi zao zisizokubalika.