1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLibya

Miili 11 ya wanaodhaniwa wahamiaji yaokolewa pwani ya Libya

8 Juni 2024

Miili 11 ya watu wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji imekutwa karibu na pwani ya Libya jana Ijumaa, Madakatari Wasio na Mipaka, wamesema.

Boti ya uokozi ya Madaktari Wasio na Mipaka, MSF
Wengi wa wahamiaji wanaojaribu kwenda Ulaya kupitia bahari ya Mediterania wanakabiliwa na kitisho cha kifo na majanga mengine wakiwa njianiPicha: Frédéric Séguin/dpa/MSF/picture alliance

Kundi hilo limeandika kupitia mtandao wa X kwamba miili hiyo ilipatikana baada ya msako wa masaa tisa uliofanywa na timu ya uokozi ya GeoBarents. 

Madaktari hao waliarifiwa juu ya miili hiyo na shirika lisilo la serikali la Ujerumani la Sea-Watch ambalo mapema jana Ijumaa lilisema liliona miili 11 ya watu ikielea majini.

Kulingana na Sea-Watch, serikali ya Libya kupitia kikosi cha uokozi kinachofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, iliamua kuiacha miili hiyo baharini. 

Makundi hayo kwa pamoja yamezilaumu nchi za Ulaya kwa vifo hivyo, kutokana na sera zake ngumu za uhamiaji.