1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Miili 40 yapatikana baada ya Israel kukamilisha operesheni

12 Julai 2024

Shirika la ulinzi wa raia Gaza limeliambia shirika la habari la AFP kuwa limepata miili 40 leo katika hatua ya awali ya kutafuta miili katika wilaya mbili za mji wa Gaza, baada ya Israel kukamilisha operesheni yake.

Miili ya Wapalestina ikipelekwa katika hospitali ya al-Ahali Baptist
Miili ya Wapalestina ikipelekwa katika hospitali ya al-Ahali BaptistPicha: Dawoud Abo Alkas/AA/picture alliance

Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal amesema miili hiyo imepatikana katika wilaya za Tal al-Hawa na al-Sinaa.

Shirika hilo na wakaazi wamesema, jeshi la Israel limeondoka baada ya makabiliano ya siku kadhaa na wanamgambo wa Hamas, ingawa hilo halijathibitishwa na jeshi la Israel.

Soma pia: Hamas yasema haijapokea taarifa kutoka kwa wapatanishi

Haya yanafanyika wakati ambapo Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan amesema hatoidhinisha ushirikiano wowote wa siku zijazo kati ya jeshi la jumuiya ya kujihami ya NATO na Israel, wakati vita vya Israel dhidi ya Hamas vinaendelea huko Gaza.

Erdogan ameyasema haya katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa X leo baada ya kukamilika kwa mkutano wa kilele wa NATO mjini Washington jana. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW