1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 60 yafukuliwa Gaza baada ya shambulizi la Israel

13 Julai 2024

Kwa mujibu wa Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal takriban miili 60 imepatikana hadi sasa, ikiwa ni pamoja na familia ambayo iliuawa kwa risasi za moto na mashambulizi ya anga walipokuwa wakijaribu kukimbia

Gaza |  Khan Younis
Wafanyakazi wa uokoaji wakiwa katika eneo liloshambuliwa na Israel huko GazaPicha: Mohammed Salem/REUTERS

Wafanyakazi wa Shirika la ulinzi wa raia huko Gaza wameendelea na shughuli ya kutoa miili kwenye majengo yaliyoporomoka na kuiondoa kwenye vifusi huku wakikusanya makumi ya Wapalestina waliouawa wiki hii na shambulio la Israel huko Gaza.

Kwa mujibu wa Msemaji wa shirika hilo Mahmud Bassal takriban miili 60 imepatikana hadi sasa, ikiwa ni pamoja na familia nzima ambao walionekana kuuawa kwa risasi za moto na mashambulizi ya anga walipokuwa wakijaribu kukimbia.

Soma zaidi. Miili 40 yapatikana baada ya Israel kukamilisha operesheni yake Gaza City

Wakati huo huo huko mjini Cairo, wapatanishi wa Misri na Qatar wanaendelea kushinikiza kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa ya mpango wa awamu ya tatu wa kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka huko Gaza.

Pendekezo hilo linaloungwa mkono na Marekani linataka kusitishwa kwanza kwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka na kuondolewa kwa wanajeshi wa Israeli kutoka maeneo yenye watu wengi huko Gaza. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW