1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili miwili yapatikana jengo lililoporomoka Marseille

10 Aprili 2023

Miili miwili imepatikana kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka katika mji wa Marseille, Ufaransa, kufuatia mripuko mkubwa.

Frankreich Marseille | Wohnhaus eingestürzt
Picha: CLEMENT MAHOUDEAU/AFP/Getty Images

Idara ya zima moto katika taarifa yake leo Jumatatu imesema kwamba zoezi hilo litachukua muda kutokana na changamoto zilizojitokeza katika kuchimbua miili hiyo.

Miili hiyo imepatikana takribani masaa 24 baada ya mripuko huo kusababisha kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne.

Taarifa rasmi ya siku ya Jumapili jioni ilisema kuwa  waokoaji walikuwa wakiwatafuta watu wanane ambao walidhaniwa kukwama kwenye vifusi.

Mamlaka katika mji huo imesema serikali bado imejitolea kikamilifu kuendelea na zoezi la utafutaji wa waathirika wa mkasa huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW