Miili ya wahamiaji yapatikana mpaka wa Tunisia-Algeria
12 Julai 2023Hayo yameelezwa na afisa mmoja wa mahakama na shahidi mwingine aliyekata kutambulishwa jina lake kwa sababu za usalama. Kulingana na msemaji wa mahakama ya wilaya ya Tozeur ya kusini mashariki mwa Tunisia, mwili wa kwanza ulipatikana siku 10 zilizopita kwenye jangwa la Hazoua na mwili mwingine ulipatikana Jumatatu ya wiki hii.
Soma pia: Wahamiaji 300 hawajulikani waliko baharini Atlantiki
Afisa huyo amesema mamlaka zimefungua uchunguzi wa "kifo cha mashaka" ili kubaini sababu za watu hao waiwli kupoteza maisha.
Wahamiaji kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara waliokuwa wakiishi kwenye mji wa Sfax wametumbukia kwenye uhasama na wenyeji baada ya kifo cha mwanaume mmoja raia wa Tunisia kilichotokea Julai 3. Mwanaume huyo alidungwa kisu wakati wa makabiliano kati ya pande hizo mbili.
Tangu wakati huo mamia ya wahamiaji wamelazishwa kuukimbia mji huo wa wamesafirishwa kwa nguvu na kupelekwa kwenye eneo la Jangwa kwenye mpaka wa Tunisia na mataifa jirani ya Algeria na Libya.