UhamiajiTunisia
Miili ya watu 9 yapatikana Tunisia baada ya boti kuzama
12 Desemba 2024Matangazo
Farid Ben Jha, msemaji wa ofisi ya mashtaka ya majimbo ya Monastir na Mahdia, amesema watu walionusurika wamewaambia maafisa kwamba boti yao ilizama baada ya kuanza safari usiku wa Jumanne katika mji wa Sfax.
Mji huo ni kituo kikuu cha wahamiaji wanaoelekea Italia. Ben Jha amesema abiria wote 42 waliokuwemo ndani ya boti hiyo wanatokea kwenye nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Watu sita bado hawajulikani walipo, na watu 27 wameokolewa. Tunisia na nchi jirani ya Libya, zimekuwa vituo muhimu vya kuondokea wahamiaji, mara nyingi kutoka nchi nyingine za Kiafrika, wanaohatarisha maisha yao kwa kuvuka Bahari ya Mediterania kwa matumaini ya kufika Ulaya kutafuta maisha bora.