1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakazi waanza kuukimbia mji wa Khartoum

20 Aprili 2023

Maelfu ya wakaazi waelezwa kuukimbia mji mkuu wa Sudan, Khartoum ambapo mashuhuda wanaliripoti hali ya kuzagaa miili ya watu mitaani na balozi zikisema zaidi ya raia 270 wameuawa katika mapigano.

Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: El-Tayeb Siddig/REUTERS

Maelfu ya wakaazi waelezwa kuukimbia mji mkuu wa Sudan, Khartoum ambapo mashuhuda wanaliripoti hali ya kuzagaa miili ya watu mitaani na balozi zikisema zaidi ya raia 270 wameuawa katika mapigano kati ya jeshi na wapiagaji wa kikosi cha cha dharura cha Rapid Support Forces  huku mapigano hayo yakionesha kutokuwa na ukomo.

Mkazi wa jiji la Khartoum,  Alawya al-Tayeb, mwenye umri wa miaka 33 amenukuliwa na Shirika la Habari la Ufaransa AFP akisema maisha katika jiji hilo hayatowezekana tena kama vita hivyo havitokuwa na ukomo.

Amesema anajaribu kuwazuia watoto wake wasiweze kuona miili ya waliuwawa mitaani, na kuongeza kuwa tayari vijana wake wameanza kuwa na tatizo la kuweweseka na hivyo watahiji matibabu.

Hatua tata ya kusitisha mapigano

Moshi wa mripuko mjini KhartoumPicha: Ahmed Satti/AA/picture alliance

Wapiganaji wa RSF walisema wameamua kuacha mapigano kwa ukamilifu kuanzia jioni ya Jana, kwa kipindi cha masaa 24, kama ilivyoamuliwa pia na jeshi. Lakini milio ya risasi iliendelea kusikia mjini Khartoum kuanzia wakati uliokusudiwa hadi usiku wa kuamkia leo (20.04.2023).

Rais wa Kenya William Ruto, ambaye ni miongoni mwa wapatanishi ameonya kuonya kuwa machafuko yanaweza kuleta hali ya kutokuwa na utulivu wa kikanda.

Ruto pia alizitaka pande  hasimu Sudan kuruhusu upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kushirikiana na mamlaka ya kikanda katika eneo la Afrika Mashariki na serikali katika kufanikisha matokeo chanya.

Vifo vinaweza kufikia watu 300

Jeshi la Sudan na mpinzani wake, kikosi kijulikanacho kama Rapid Support Forces, wamekuwa mapigano kwa siku takribani tano ambayo yamesababisha vifo vya karibu watu  300, kwa rekodi za Shirika la afya la Umoja wa Mataifa.

Viongozi wa Jumuiya ya Kikanda IGAD Jumapili walitoa azimio la kutaka kusitishwa uhasama nchini Sudan, ambayo kwa sasa ni mwenyekiti wa kundi hilo la kikanda. Ruto wa Kenya alisema hali nchini Sudan inabadilika na kuwa tishio kwa amani na usalama wa kikanda na kimataifa na kuonesha  na kuchukizwa na hilo.

Sudan inapakana na Ethiopia, Eritrea, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Libya na Misri.

Mataifa yameanza juhudi ya kuwanusuru raia wao

Mkurugenzi wa Taasisi yenye kuhusika na utafiti wa migogoro katika eneo la Pembe ya Afrika-International Crisis Group, Alan Boswell alisema mapigano hayo yanaweza kuwa na athari katika eneo hilo.

Kenya inapanga kuwahamisha takriban raia wake 3,000 wanaoishi Sudan, fikra kama hizo zipo hata nje ya mipaka ya Afrika.Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema hali ilivyo nchini Sudan ni ya hatari kwa raia wa taifa hilo na wageni. Ujerumani ina wajibu wa kuwanusuru raia wake, pamoja na raia wa mataifa mengine kuondoka nchini humo.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari alisema wanahisi wanawajibu wa kufikiria uwezekano wa watu hao kuondoka nchini humo na kusaidia utekelezaji wake.

soma zaidi:RSF wakubali kusitisha mapigano kwa saa 24

Awali jarida la hapa Ujerumani, Spiegel liliandika kuwa jeshi la Ujerumani limesitisha kazi zake za ulinzi wa amani na kusaidia uokozi wa takribani watu 150 kutoka Sudan, kufuatia mapigano yanayoendelea.

Vyanzo: DPA, AFP, RTR

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW