Miili zaidi ya 30 yagundulika kwenye kaburi la pamoja Kenya
25 Machi 2026
Hayo ni katika kile kinachoelezewa kuwa mtafaruku mpya wa kijamii kufuatia mtiririko wa matukio kama hayo ya kugunduliwa makaburi ya pamoja kila baada ya muda kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.
Eneo la makaburi huko Kericho limegeuka kuwa eneo la uhalifu baada ya miili 32 kufukuliwa kutoka kwenye kaburi la pamoja.
Kukamilika kwa kazi ya kufukua maiti
Maafisa wa upelelezi wa mauaji kutoka makao makuu ya DCI waliokuwa wamekita kambi eneo hilo walianza zoezi la ufukuaji wa miili, ambalo lilikamilika saa moja jioni jana.
Iliripotiwa awali kuwa miili 14 ilidaiwa kuzikwa katika eneo hilo Ijumaa iliyopita. Kufuatia amri ya mahakama iliyoruhusu kufukuliwa kwa kaburi hilo la siri, matokeo yalikuwa ya kushtua zaidi. Daktari wa serikali, Richard Njoroge anasema "Miili hiyo ilikuwa imepakiwa ndani ya magunia. Tulipata watu wazima 7 na watoto 25. Kwa jumla tuna miili 32, na pia tulipata sehemu 6 za miili miguu 4 na mikono 2. Tutazichambua ili kubaini kama zinatoka kwa mtu mmoja.”
Utaratibu wa uchunguzi wa maiti
Baada ya zoezi la ufukuaji kukamilika, sasa mwelekeo unaelekezwa kwenye uchunguzi wa maiti unaotarajiwa kubaini chanzo cha vifo hivyo. Njoroge anaongeza kusema "Baadhi zinaonekana kana kwamba zimetoka katika mochari na nyingine hospitalini. Hata hivyo, tutathibitisha hilo baada ya kukamilisha zoezi la uchunguzi wa maiti. Sitasema tutaanza uchunguzi huo lini. Si zoezi rahisi na lazima lifanywe kwa umakini mkubwa.”
Waliokuwepo kushuhudia zoezi hilo ni wanaharakati wa haki za binadamu ambao wameeleza wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa visa vya makaburi ya pamoja. Wanaharakati Hussein Khalid (Vocal Africa), Fredrick Odhiambo.
Ugunduzi huu unaibua maswali kuhusu walikokuwa watu hao, namna ya siri iliyotumika kuwazika, na ukosefu wa ushirikishwaji wa umma.