1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miji kadhaa ya Ujerumani kufanya maandamano dhidi cha AFD

2 Februari 2025

Makundi mbalimbali katika miji ya Ujerumani yametangaza kufanya maandamano leo Jumapili dhidi ya chama cha mrengo mkali wa kulia cha AFD. Maandamano makubwa yanatarajiwa katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.

Berlin I 2025 | maandamano
Makundi mbalimbali katika miji ya Ujerumani yametangaza kufanya maandamano Jumapili Picha: Tobias Schwarz/AFP/Getty Images

Makundi mbalimbali katika miji ya Ujerumani yametangaza kufanya maandamano leo Jumapili dhidi ya chama cha mrengo mkali wa kulia cha AFD. Maandamano makubwa yanatarajiwa katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.

Wakati vyama vyote vya Ujerumani vikiahidi kutofanya kazi na AfD, Chama cha CDU/ CSU mapema wiki hii kilitegemea kura za chama cha AfD kinachopinga wageni kupitisha hoja ya kudhibiti uhamiaji na sera za mipakani. Hatua hiyo ilikosolewa na Kansela Olaf Scholz na kuzusha hofu na hasira ya Umma.

Soma zaidi: Israel yasema imewaua magaidi huko Ukingo wa Magharibi

Maandamano hayo yanaelekezwa dhidi ya kambi ya upinzani ya kihafidhina ambayo baada ya hoja yao kupita siku ya Jumatano, waliwasilisha muswada rasmi wa uhamiaji ambao hata hivyo ulikataliwa na bunge la Ujerumani, Bundestag, siku ya Ijumaa.

Mbali na Berlin, maandamano yanatarajiwa pia kufanyika kwenye miji ya Kassel,Regensburg, Ulm na Nuremberg.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW