1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Miji ya Darfur yashambuliwa huku vita vya Sudan vikisambaa

14 Juni 2023

Mapigano yameitikisa miji tete magharibi mwa Sudan leo, wakati mzozo wa kuwania udhibiti kati ya jeshi la serikali na kikosi cha wapiganaji cha RSF ukitanuka na idadi ya waliokimbia makazi yao ikipindukia milioni mbili.

Sudan Konflik l Region Darfur, niedergebrannte Bankfiliale im Süden von Khartum
Picha: -/AFP via Getty Images

Vita kati ya jeshi na RSF vimesababisha mzozo wa kiutu wa kibinadamu mjini Khartoum, pamoja na miji mingine ikiwemo El Obeid, Nyala, El Fashir na El Geneina, ambako zaidi ya watu 1,100 wameuawa.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Al-Hadath kutokea mji wa El Geneina, huku milio ya risasi na makombota ikisikika, gavana wa jimbo la Darfur Magharibi Khamis Abubakar, alitoa wito wa uingiliaji wa kimataifa katika kile alichokiita mauaji ya kimbari.

Soma pia: Miili 180 yazikwa bila ya kutambuliwa kufuatia mapigano makali Sudan

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alielezea wasiwasi wa katibu mkuu huyo juu ya kuongezeka kwa vurugu zenye mwelekeo wa ukabila pamoja na ripoti za vurugu za kingono.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW