1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miji ya Vienna na Cologne yajipanga kitisho cha mashambulizi

25 Desemba 2023

Polisi kwenye mji mkuu wa Austria, Vienna, na mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Cologne, wamesema wanaimarisha ulinzi kufutia dalili za uwezekano wa kutokea mashambulizi wakati wa sherehe za sikukuu ya Krismasi.

Ujerumani | Magari ya polisi mbele ya Kanisa Kuu mjini Cologne.
Polisi wameongeza ulinzi kwenye Kanisa Kuu mjini Cologne. Picha: Roberto Pfeil/dpa/picture alliance

Mamlaka za miji hiyo zimesema zimepata taarifa kuhusu mipango ya kufanywa shambulizi na kundi moja la itikadi kali kwenye kanisa kuu mjini Cologne na jingine mjini Vienna.

Idara ya Usalama wa Taifa nchini Austria tayari imewakamata watu wanne katika uchunguzi wake juu ya mtandao wa kiislamu unaotuhumiwa kula njama za kutaka kufanya mashambulizi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser, amesema vyombo vya usalama vinachukua hatua zote kudhibiti uwezekano wa kutokea mashambulizi na ameapa kwamba jamii ya Wajerumani haitatishwa kuacha kusherehekea Krismasi kutokana na vitimbi vya makundi ya itikadi kali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW