1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MILAN ; Berlusconi alazwa hospitali

27 Novemba 2006

Berlusconi yuko katika hospitali mjini Milan ambapo anachunguzwa kwa matatizo madogo ya moyo baada ya kuzirai katika mkutano wa kisiasa.

Televisheni ya Italia imemuonyesha Berlusconi akizirai mikononi mwa wasaidizi wake wakati akihutubia wafuasi wake huko Montecatini Terme karibu na mji wa Florence.

Berlusconi ambaye anaongoza upinzani wa mrengo wa kulia wa wastani wiki iliopita alifikishwa mahkamani kwa madai ya udanganyifu na kuhalilisha fedha zilizopatikana kwa njia isio ya halali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW