1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milango ya Ujerumani iko wazi kwa Nigeria: Steinmeier

12 Desemba 2024

Rais Frank-Walter Steinmeier asifu mageuzi ya kiuchumi ya Nigeria, katika ziara yake Abuja baada ya mkutano wake na mwenyeji wake Bola Tinubu.

Frank-Walter Steinmeier na Bola Tinubu
Rais Frank-Walter Steinmeier akiitembelea NigeriaPicha: Ubale Musa/DW

Rais  Frank-Walter Steinmeier amesema  milango ya Ujerumani iko wazi kwa Nigeria kibiashara. Kiongozi huyo wa Ujerumani ameyasema hayo kwenye ziara yake Abuja, Nigeria. 

Nigeria ndio kituo cha kwanza cha ziara ya rais wa Ujerumani-Frank-Walter Steinmeier ambako aliwasili jana Jumatano mji mkuu Abuja. Amemwambia mwenyeji wake rais Bola Tinubu kwamba milango ya nchi yake Ujerumani iko wazi kwa wafanyabiashara wa Nigeria.

Nigeria yafanya mageuzi ya kiuchumi

Kwa upande wake Bola Tinubu amesisitiza kwamba Nigeria imeanzisha mageuzi yatakayoleta ufanisi wa kiuchumi katika kipindi cha hivi karibuni na kuyataja baadhi ya mageuzi hayo kuwa ni pamoja na kupunguza ukiritimba na kufanya mageuzi ya kodi.

Frank-Walter Steinmeier pamoja na Bola TinubuPicha: Ubale Musa/DW

Rais Steinmeier amezisifu juhudi hizo  za Nigeria akisema mageuzi yanatazamwa na jumuiya ya wafanyabiashara nchini Ujerumani kama hatua ya kuimarisha mahusiano na wawekezaji.

'' Tunao pia ushirikiano wa muda mrefu na  Nigeria katika sekta ya nishati ambao Ujerumani imewahi kuwa nao, na kwahivyo kwa muda mrefu tumejenga bodi ya ushirikiano ambayo inahusika  kuratibu mipango ya baadae ya maendeleo katika sekta ya masoko ya nishati na mahitaji yanayoibuka linapohusu suala la ulinzi wa mazingira.''

Ujerumani yalenga kuimarisha ushirikiano kiuchumi

Hii leo rais huyo wa Ujerumani anatarajiwa kufanya mazungumzo zaidi mjini Lagos yatakayojikita juu ya suala la ushirikiano wa kiuchumi kabla ya hapo baadae kuendelea na ziara yake barani Afrika akielekea Afrika Kusini na Lesotho.

Nigeria nchi yenye idadi ya watu kiasi milioni 220 ni mashirika wa pili mkubwa wa kibishara wa Ujerumani katika kanda ya Kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.

Nchi hiyo hatahivyo pamoja na utajiri wa mafuta iliyonao inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili sasa.

Wanigeria hawayataki mageuzi ya kiuchumi ya rais Tinubu, wakilaumu kwamba yamechangia kuleta mfumko mkubwa wa bei ambao umesababisha kupanda kwa kiwango cha kutisha gharama ya maisha.

Frank-Walter Steinmeier akiwa Abuja NigeriaPicha: Ubale Musa/DW

Na juu ya hilo kuendelea kuongezeka kwa upungufu wa mafuta na kukatika kwa umeme ni masuala yanayozidi kurudisha nyuma ukuaji wa kiuchumi.

Jumatano rais Tinubu aligusia juu ya uwezekano wa kuweko ushirikiano na Ujerumani katika sekta ya gesi majimaji asili pamoja na nishati jadidifu huku rais wa Ujerumani Steinmeier akizungumzia suala la Hydrojeni.

Steinmeier pia alifanya mazungumzo hiyo jana na Omar Touray ambaye ni rais wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika-ECOWAS ambayo ina wanachama 15 na ambayo katika miaka ya hivi karibuni imeonesha kudhoofishwa na hatua ya kujiondowa kwa Niger,Mali na BurkinaFaso.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW