1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milio ya risasi yasikika karibu na Ikulu ya Guinea

27 Septemba 2024

Milio ya risasi ilisikika jana Alhamisi karibu na majengo ya Ikulu kwenye mji mkuu wa Guinea, Conakry, na jeshi lilichukua hatua ya kuweka vizuizi vya muda katikati ya mji huo na kuamuru watu kuondoka.

Conakry, Guinea | Mamady Doumbouya
Kiongozi wa kijeshi wa Guinea Mamady DoumbouyaPicha: Cellou Binani/AFP

Milio ya risasi ilisikika jana Alhamisi karibu na majengo ya Ikulu kwenye mji mkuu wa Guinea, Conakry, na jeshi lilichukua hatua ya kuweka vizuizi vya muda katikati ya mji huo na kuamuru watu kuondoka.

Soma: Utawala wa kijeshi Guinea waamuru kuvunjwa kwa serikali

Mwandishi mmoja wa habari aliyekuwa mita chache kutoka ikulu ya nchi hiyo ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba alisikia milio ya risasi na kuwaona watu wakitimua mbio kwa mshtuko.

Ripoti pia zinasema wanajeshi waliojihami kwa silaha walionekana wakipiga doria kwenye mitaa ya mji mkuu Conakry. Chanzo kimoja cha kidiplomasia kilicho karibu na kiongozi wa Guinea kimesema wanajeshi 11 walioasi waliwafyetulia risasi walinzi wa ikulu lakini walizidiwa nguvu. Kimearifu kwamba watatu kati yao wameuwawa na wanane wengine wametiwa nguvuni na kusisitiza kwamba hali imedhibitiwa.

Taifa hilo la Afrika Magharibilimekuwa likiongozwa na utawala wa kijeshi tangu kupinduliwa kwa Rais Alpha Konde mwaka 2021.  Kiongozi wa nchi hiyo Kanali Mamadi Doumbouya alimpindua Konde akisema alikuwa na lengo la kuizuia Guinea kutotumbukia kwenye machafuko baada serikali ya Konde kushindwa kutimiza ahadi za wakati wa kampeni. 

Jumuiya ya Kiuchumi ya kanda hiyo ECOWAS imejaribu kushinikiza kuharakishwa kipindi cha mpito na kurejeshwa utawala wa kiraia na hivi sasa uchaguzi umepangwa kufanyika mwaka 2025.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW