SiasaUkraine
Milipuko miwili yautikisa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv
11 Novemba 2023Matangazo
Waandishi habari wa shirika la AFP wameripoti kuona moshi angani muda mfupi kabla ya kuanza kulia kwa ving´ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga.
Meya wa mji huo Vitali Klitschko ameandika kwenye ukurasa wa Telegram kuwa milipuko hiyo ilikuwa ni makombora yaliyoulenga mji huo lakini yalidunguliwa na mifumo ya ulinzi ya Ukraine.
Hakuna ripoti zozote za majeruhi kutokana na kisa hicho. Mji huo mkuu wa Ukraine umeshuhudia karibu wiki nane za utulivu licha kuendelea kwa vita upande wa mashariki.
Mnamo Spetemba 21 mifumo ya ulinzi ya Ukraine iliyotolewa kwa sehemu kubwa na mataifa ya magharibi ilidungua kombora moja ambalo mabaki yake yaliyoanguka yaliwajeruhiwa watu 7 mjini Kyiv.