1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Mimi ndiye bosi," Trump awaambia viongozi wa G7

17 Juni 2026

Kauli ya Donald Trump kwamba "Mimi ndiye bosi" imeiba show katika mkutano wa G7 nchini Ufaransa, huku ushawishi wake ukitawala mijadala ya Iran, Ukraine na uchumi wa dunia.

G7 Évian-les-Bains 2026 | Donald Trump akikutana na Abdel Fattah al-Sisi kandoni mwa mkutano wa G7
Baada ya makubaliano ya Iran, Trump aliingia G7 kama mtu aliyeshinda uchaguzi wa darasa. "Mimi ndiye boss!"Picha: Julia Demaree Nikhinson/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amewavutia tena viongozi wa mataifa tajiri ya G7 baada ya kuingia katika kikao cha mwisho cha mkutano wa kilele nchini Ufaransa kwa kauli iliyozua kicheko na mjadala.

"Mimi ndiye bosi," Trump alisema alipokuwa akiingia katika kikao cha Jumatano asubuhi huku viongozi wengine tayari wakiwa wameketi.

Kauli hiyo ilimlenga mwenyeji wa mkutano huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alionekana kuipokea kwa utani. Macron alimsalimia Trump kwa kumuuliza hali yake, naye akajibu kwa kifupi, "Nzuri, asante", kabla ya kuketi.

Rais Donald na viongozi wengine wa G7 wakimsikiliza Waziri Mkuu wa India Narendra wakati wa kikao cha Kujenga ushirikiano mpya na kurejesha mshikamano wa kimataifaPicha: ANI/DPR PMO

Uwepo wa Trump umetawala kwa kiasi kikubwa mkutano huo wa siku tatu uliofanyika katika mji wa Evian kandokando ya Ziwa Geneva. Hali hiyo imechangiwa na makubaliano ya awali aliyosaidia kufikiwa kati ya Marekani na Iran pamoja na siku yake ya kuzaliwa ya 80 iliyoadhimishwa wakati wa mkutano huo.

Kwa viongozi wa Ufaransa, hatua ya Trump kuhudhuria mkutano wote hadi mwisho inachukuliwa kuwa mafanikio ya kidiplomasia. Katika mkutano uliopita wa G7 nchini Canada, Trump aliondoka kabla ya shughuli kukamilika.

Aidha, tofauti na ilivyotarajiwa na baadhi ya wachambuzi, Trump ameunga mkono taarifa ya pamoja ya G7, hatua ambayo imeepusha mvutano uliowahi kushuhudiwa katika mikutano ya nyuma.

Kabla ya kurejea Washington, Trump anatarajiwa kuwa mgeni wa Macron katika chakula cha jioni kitakachofanyika katika Kasri la Versailles nje ya Paris.

Hata Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alikumbushwa kuwa Trump bado 'ndiye Boss'!Picha: Ukrainian Presidential Press Service/AFP

Ikulu ya Ufaransa imekuwa makini kupunguza taswira kwamba Macron anajaribu kujikurubisha mno kwa Trump. Rais huyo wa Ufaransa tayari amesisitiza kwamba hafla hiyo haitakuwa chakula cha jioni cha kifahari wala sherehe maalumu, bali sehemu ya shughuli za kawaida za kidiplomasia.

Hata hivyo, kauli ya Trump ya "Mimi ndiye bosi" imeongeza sura nyingine katika mkutano ambao tangu mwanzo umekuwa ukigubikwa na ushawishi wake katika masuala ya Iran, Ukraine na uchumi wa dunia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW