1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mionzi ya nyuklia imezidi Japan

17 Machi 2011

Mafuta katika kinu cha nyuklia cha Fukushima yanaonekana kukaribia kuyeyuka baada ya moto mwingine kuzuka.

Kiwanda cha nyuklia cha Fukushima Dai-ichi kilichpo Okumamachi, kaskazini mwa Japan.Picha: AP

Wasimamizi wa kinu cha nyuklia cha Fukushima nchini Japan wamesema watajaribu tena hii leo kutumia helikopta kuvipoesha vinu hivyo vilivyoshika moto.

Athari ya tetemeko la ardhi na tsunami Japan.Picha: Kyodo News/AP/dapd

Moto mwingine uliozuka hapo jana katika kinu hicho ulilazimisha kuhamishwa wafanyakazi kwenye. Mafuta katika kinu cha nyuklia cha Fukushima yanaonekana kukaribia kuyeyuka baada ya mfululizo wa miripuko kufutia tetemeko la ardhi lililoyaharibu majenereta ya kuvipoesha vinu hivyo.

Wakati huohuo msimamizi mkuu wa nyuklia Marekani ameonya kuwa sehemu ya maji ya kupoesha vyuma vya mafuta kwenye kinu kimoja, huenda yakawa yamekauka na katika kinu kingine yanavuja. Gregory Jaczko ambaye ni mkuu wa tume ya usimamizi wa nyuklia Marekani, hapo jana alisema kuwa viwango vya mionzi ya nyuklia vipo juu mno.

Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki IAEA, Yukiya Amano, anatarajiwa kuelekea Japan hii leo. Aliweza kuitaja hali nchini humo kuwa mbaya. Mamia kwa maelfu ya watu wameachwa bila makaazi. Maji na Chakula ni haba. Karibu nyumba milioni moja hazina umeme na huku watu milioni moja na nusu hawana maji yanayotoka miferejini.

Mwandishi:Maryam Abdalla/ AFP, Rtrs

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi