1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
HistoriaAfrika

Kwa nini Afrika bado inapigania mipaka ya wakoloni?

30 Desemba 2023

Wakoloni waliaondoka Afrika zaidi ya karne nzima iliyopita, lakini mipaka iliyochorwa kwenye Mkutano wa Berlin kati ya mwaka 1884 na 1885 bado iko kama ilivyokuwa hadi leo - na imekuwa na matokeo mabaya.

Mfululizo wa makala hizi za za Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani unatayarishwa na DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani (AA). Ushauri wa masuala ya historia umetolewa na Profesa Lily Mafela, Profesa Kwame Osei Kwarteng na Reginald Kirey.
Mfululizo wa makala hizi za za Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani unatayarishwa na DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani (AA). Ushauri wa masuala ya historia umetolewa na Profesa Lily Mafela, Profesa Kwame Osei Kwarteng na Reginald Kirey.Picha: Comic Republic

Kwa nini Ukanda wa Caprivi ni alama ya uchoraji ramani wa kikoloni?

Ukanda wa Caprivi ni mojawapo ya maeneo yenye muonekano mbaya kabisa kwenye ramani na ni sehemu ya Namibia ya sasa.

Unaonekana kama mpini wa kisu na una ina mistari ya moja kwa moja inayofanana kwa umbali wa kilomita 30 inayopitia kwenye savana na mifumo ya mito. Mkubwa kabisa ni Mto Zambezi.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Pili

This browser does not support the audio element.

Ukanda huu uliundwa na wanadiplomasia wa Kizungu wakiwa na haraka ya kupata maeneo kwa ajili ya mataifa yao bila ya kusababisha mgogoro na mataifa mengine jirani ya Ulaya. Wachache walikuwa wamewahi kulitembelea eneo hilo walilokuwa wakigawana, lakini walitaka kuyazuwia mataifa mengine ya kikoloni kuyachanyaga maeneo zaidi kuelekea Mashariki na Magharibi au Kaskazini na Kusini.

Vipi Ukanda wa Caprivi uliundwa?

Baada ya Mkutano wa Berlini wa mwaka 1884, Ujerumani ya Afrika Kusini Magharibi ilitenganishwa na Ujerumani ya Afrika Mashariki na Mahamiya ya Uingereza ya Bechuanaland Botswana, Rhodesia ya kaskazini na kusini (Zambia na Zimbabwe za leo). 

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani

02:47

This browser does not support the video element.

Kwa hivyo, mnamo mwaka 1890, Kansela Leo von Caprivi alikubaliana na Uingereza kupata kipande cha ardhi kitakachowapa Wajerumani fursa ya kupitia Ujerumani ya Afrika Kusini Magharibi kwenda Mto Zambezi, ambao Ujerumani ulijuwa kuwa unamwaga maji yake Afrika Mashariki.

Soma zaidi: Kampuni ya Woermann ilivyousafirisha ukoloni wa Ujerumani

Kwa kupatiwa njia hii ya biashara, Ujerumani ilikubali kutambua madai ya Uingereza kwa Zanzibar na Pemba, visiwa vilivyo kwenye mwambao wa Ujerumani ya Afrika Mashariki, nayo ingelipatiwa kituo kidogo cha jeshi la majini kwenye kisiwa cha Heligoland kilichopo Bahari ya Kaskazini kwenye mwambao wa Ujerumani.

Makubaliano haya yalikuja kufahamika kama Mkataba wa Heligoland-Zanzibar wa mwaka 1890 kati ya Uingereza na Ujerumani.

Tatizo lilikuwa lipi?

Sasa Ujerumani ilikuwa na himaya ya nne kwa ukubwa duniani, lakini umbali wa kilomita 40 upande wa mashariki pale Ukanda wa Caprivi ulipoishia, maporomoko makubwa ya maji, Mosi-oa-Tunya ama Victoria Falls, yalichomoza.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Nne

This browser does not support the audio element.

Maajabu haya ya kimaumbile yaliufanya Mto Zambezi uwe hauwezi kuvuukika, na mpango wa Ujerumani ukakwama hapo.  

Yapi yamekuwa matokeo ya mkwamo huu wa kijiografia?

Zaidi ya makabila sita yanayozungumza zaidi ya lugha 12 yakajikuta mara moja yakiwa chini ya mamlaka nne tafauti za kikoloni.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Utwaaji wa ardhi

01:59

This browser does not support the video element.

Wakati wa ukoloni Ukanda wa Caprivi kwa kiasi kikubwa ulikuwa salama, hasa kwa sababu Ujerumani haikuwa na maslahi makubwa kwenye eneo hilo.

Lakini hali hiyo ilikuja kubadilika pale Ujerumani ilipopoteza makoloni yake kwa Mkataba wa Versaillles wa mwaka 1919.

Namibia, au Ujerumani ya Afrika Magharibi, ikawekwa chini ya amana ya Afrika Kusini, kwa matarajio ya kuja kuwa huru siku zijazo. Lakini hilo kamwe halikutokea.

Badala yake, Afrika Kusini ikaanzisha sera zake za ubaguzi wa rangi, na kuiwekea Caprivi utawala wa kibaraka.

Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kwanza

This browser does not support the audio element.

Na kutoka miaka ya 1960, kutokana na kuwepo kwake kwenye eneo la kimkakati kijiografia na kisiasa, Ukanda wa Caprivi ukawa kitovu cha vita na makabiliano kati ya jeshi la Afrika ya Kusini na wapiganaji waliokuwa wakifanya uvamizi wa mipakani uliohusiana na Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Angola, Vita vya Mpakani na Vita vya Msituni vya Rhodesia. 

Soma zaidi: Ukosefu wa imani kwa chanjo za Magharibi ulivyozalika wakati wa ukoloni

Migogoro hii mitatu tafauti haikuhusiana kabisa na watu waliokuwa wanaishi kwenye Ukanda huo na ilikuwa inahusiana kikamilifu na mataifa ya kigeni yaliyokuwa yakijaribu kutwaa udhibiti wa eneo hilo.

Mapigano yalisimama mwishoni mwa miaka ya 1990 baada ya jaribio la muda mfupi la wenyeji wa Caprivi kujitenga na Namibia huru mwaka 1997 kushindwa.

Mizozo ipi mingine ipo juu ya mipaka ya wakoloni kwenye makoloni ya zamani ya Ujerumani?

Mgogoro uliripuka kwenye miaka ya 2000 kati ya Kameruni na Nigeria zikiwania ghuba ya Bakassi.

Raia wa Nigeria walishaishi kwa miaka mingi kwenye ardhi ambayo Kameruni inadai ni yake kwa kutegemea makubaliano ya zama za kikoloni.

Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Tatu

This browser does not support the audio element.

Mapigano ya hapa na pale bado yanatokea hadi sasa, licha ya Mahakama ya Haki ya Kimataifa kutoa uamuzi unaoipa haki hiyo Kameruni.

Togo, ambayo inapakana na Ghana ya sasa, pia iligawanywa baina ya Ufaransa na Uingereza mwaka 1919, pamoja na mpaka wa kubuni.

Hili lilikataliwa na wenyeji wa jamii ya Ewe, ambao sasa walijikuta kwenye nchi mbili tafauti. "Togoland ya Muingereza" au Togoland Maghabiri iliunganishwa na Ghana baada ya kura ya mwaka 1956.

Hata hivyo, mikoa yenye wakaazi wengi wa jamii ya Ewe ilipiga kura ya kuamua kusalia chini ya amana ya Umoja wa Mataifa.

Soma zaidi: Uhusiano baina ya ugozi wa zama za ukoloni na unazi

Hadi hivi leo, baadhi ya makundi ya Ewe yanadai kuwa na nchi yao huru, na serikali ya Ghana imeongeza ukandamizaji wake dhidi ya wanaharakati kupitia kamatakamata na kuweka wanajeshi wengi kwenye eneo hilo.

Na kwa Tanzania, Mkataba wa Heligoland-Zanzibar wa mwaka 1890 uliounda Ukanda wa Caprivi umesababisha pia mzozo wa muda mrefu na Malawi inayodhibiti Ziwa Malawi - ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa.

Pande hizo mbili zinabishana juu ya ulipo mpaka halisi. Kimsingi, kutokana na Mkataba huo, mpaka unapita kwenye ufukwe wa mto ndani ya Tanzania.

Soma zaidi: Quane Martin Dibobe: Kutoka maonesho hadi mwanaharakati dhidi ya ukoloni

Lakini Tanzania inahoji kwamba mpaka lazima uendane na mipaka mingine na makubaliano yanayohusu maziwa, ambapo mpaka huwa katikati ya maji.

Mizozo hii miwili isiyopatanishika ilikuwa kimya hadi mwaka 2011, pale Malawi iliporuhusu shughuli za utafutaji mafuta kwenye eneo la ziwa ambalo Tanzania inadai ni lake.

Mfululizo wa makala hizi za za Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani unatayarishwa na DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani (AA). Ushauri wa masuala ya historia umetolewa na Profesa Lily Mafela, Profesa Kwame Osei Kwarteng na Reginald Kirey.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW