Miripuko na majibizano ya risasi vyasikika tena Khartoum
22 Mei 2023Makubaliano hayo ya usitishwaji mapigano yalifikiwa mwishoni mwa wiki huko Jeddah nchini Saudi Arabia. Jana Marekani na Saudi Arabia zilitangaza kwamba makubaliano ya kusitisha vita kati ya kambi mbili zinazopigana nchini Sudan yataanza usiku wa leo, kutoa nafasi kwa msaada wa kibinadamu kuwafikia raia wa Sudan.
Pande zote mbili kwenye mgogoro zilithibitisha kwamba zitaheshimu makubaliano hayo yaliyopongezwa pia na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya maendeleo ya ushirikiano wa nchi za Mashariki mwa Afrika, IGAD.
Soma pia: Pande mbili hasimu zakubaliana kusitisha mapigano kwa wiki moja Sudan
Mpaka sasa kiasi watu 1,000 wameuwawa na zaidi ya milioni 1 wameachwa bila makaazi kufuatia mapigano ya zaidi ya wiki tano,yaliyoitumbukiza kwenye janga la kibinadamu nchi hiyo.