Miripuko yasikika katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum
7 Novemba 2025
Mkaazi mmoja wa Omdurman, ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina kwamba waliamshwa karibu saa nane usiku kwa vishindo vya miripuko karibu na kambi ya kijeshi ya Wadi Sayidna.
Mkaazi mwingine anasema alisikia milio ya droni mwendo wa saa kumi alfajiri kabla ya mripuko kusikika karibu na kituo cha umeme, na kusababisha kukatika kwa nguvu za umeme katika eneo hilo.
Jeshi la Sudan na RSF hazijatoa taarifa kuhusu mashambulizi
Hakukuwa na ripoti za haraka za majeruhi.
Jeshi la serikali na RSF bado hawajatoa tamko kuhusu mashambulizi hayo.
Wakati huo huo, Muungano wa Madaktari wa Sudan umesema kuwa RSF jana ilishambulia kwa makombora hospitali katika mji unaozingirwa wa Dilling huko Kordofan Kusini na kuwajeruhi watu kadhaa, ambapo baadhi yao wako hali mahututi.