Miripuko yauwa watatu Burundi
21 Septemba 2021Matangazo
Matukio hayo ambayo yametokea jioni ya Jumatatu yameripotiwa na polisi na vyombo vya habari vya taifa hilo.
Mashambulizi ya Bujumbura yanafanyika baada ya jengine kutokea katika mji mkubwa wa Gitega, ambako watu wawili waliuwawa na mfululizo wa mizinga iliyolenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa taifa hilo usiku wa Jumamosi.
Afisa wa polisi aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema ameshuhudia mtu mmoja akipoteza maisha mjini Bujumbura na wengine 29 wakijeruhiwa, baadhi yao vibaya sana.