1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misaada bora ya maendeleo

3 Septemba 2008

Mkutano wa jinsi ya kutumiwa bora misaada ya maendeleo na usawa wa kijinsia Accra.

Vipi msaada wa maendeleo unaweza kutumika bora ?

Hilo ndilo swsali kuu linalojadiliwa katika Jukwaa maalumu la majadiliano ya hadi ya juu mjini Accra,Ghana kuanzia juzi hadi hii leo,Septemba 4.

Wanawake wanahofia kuwa muongozo mpya uliotoka utaongoza kufutwa kwa miradi ya kuwasaidia akina mama .

Akina mama wanataka kusikilizwa sauti zao tena kwa nguvu zaidi kuliko ilivyofanyika hadi sasa.

Katika jukwaa hilo mjini Accra linalozungumzia matumizi bora ya misaada ya maendeleo lililoandaliwa na Shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD,akina mama walijiwinda pia kuona sauti zao zinasikizwa na msimamo wao wanaouchukua unatiwa maanani.

Zaidi ya wajumbe 200 wanawake kutoka mashirika ya kimataifa yasio ya serikali-NGOS- walikutana kandoni mwa mkutano hasa kwa jukwaa la wanawake mjini Accra,Ghana.Jukwaa lao liliandaliwa na Kituo kinachotetea haki za akina mama-Network for Women*s rights.

Miongoni mwa wafadhili wake ni shirika la wanawake la Umoja wa mataifa INIFEM.

Dai lao kuu ni hili:Mwongozo uliotolewa Paris na misingi ya kufnya kazi bora zaidi kwa misaada ya maendeleo unapaswa kuzingatia zaidi kuliko ilivyofanyika hadi sasa maswali ya jinsia na hasa yale ya wanawake .

Idadi ya wanahudhuria kikao hicho cha akina mama ni mara 2 zaidi kuliko ilivyotarajiwa na hivyo ikaamuliwa kuhamia kwenye hotel yenye ukumbi mkubwa wa mkutano.

Kwa kweli, mtu angefaa kuridhika na matokeo ya kikao hicho cha akina mama mjini Accra.Kwani, akina mama hao kutoka nchi mbali mbali na mashirika mbali mbali yasio ya kiserikali walijadiliana mengi mnamo miezi iliopita kimkoa ili kujiandaa kwa jukwa hili la Accra.Halafu wakasoma Tangazo la Paris na nyaraka zaidi zinazoshikamana na Tangazo hilo.halafu wote kwa pamoja wakadai kuwa maswali ya akina mama na ya jinsia -yaani juhudi za kuleta haki zaidi kati ya wanawake na wanaume ndio biramu mpya wa misaada ya maendeleo mbali na kutetea haki za binadamu na usafi wa mazingira.

Mdundo huu unavutia anasema bibi Rose Mensah-Kutin wa chama cha maendeleo cha Ghana ABANTU kwa ufupi.lakini kusisitiza swali la jinsia kuwa mojawapo ya maswali muhimu ya wsakati huu haikuwa rahisi hivyo:

"Ukilizingatia barabara Tangazo la Paris na Agenda yake ya kuifanya misaada kufanyakazi barabara utagundua kwamba swali la jinsia limeangaliwa si la kimsingi.Na kwa kuwa linachukuliwa kuwa si la kimsingi,hakuna hatua maalumu za kushughulikia kazi ya kuleta usawa wa kijinsia.Na hii inatatanisha.Tuukitarajia hayo kufanyika tulipozungumzia swali hilo....."

Alitetea Rose Mensah-kutin.

Kwamba Tangazo la Paris juu ya jinsia na mada zinazowahusu wanawake lilikua la juu juu tu,anahisi hivyo pia Florence Ebam Etta. Yeye ni mwenyekiti Kituo cha Afrika cha kutathmini usawa wa kijinsia na maendeleo (AGDEN) kwa ufupi kikiwa na makao yake mjini Nairobi,Kenya. Pamoja na mashirika mengine ya akina mama, kituo hiki pia kilihudhuria mkutano wa Accra.

Anasema:

"Tunachosema kwa mfano-kiwango cha kushiriki kwa wanaume na wanawake katika kutunga mipango ya maendeleo ya taifa na mikakati yake ichukuliwe kuwa kiyoo cha kuonesha.Tunasema pia:je, tunaweza kujipatia kiwango au daraja ya uwakilishi wa kutetzewa haki za binadamu za akina mama na katika mikataba ya kimataifa katika nyaraka za Taifa...."

Anachodai Florence Ebam Etta ni kuwa, mipango ya maendeleo ya kitaifa haizingatii mara nyingi maswali ya jinsia.Ukiiuliza idara za mipango ya maendeleo ya kitaifa ya idara za wizara mbali mbali utaambiwa :"tunagharmia miradi ya kijami kama afya na elimu.

Mkutano huu juu ya matumizi bora ya misaada ya maendeleo mjini Accra,unamalizika leo,iwapo umesikia sauti za akina mama au la,yafaa kusubiri kuona.