1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misaada kwa maendeleo endelevu

7 Septemba 2016

Mashirika ya kutoa misaada ya 'Welthungerhilfe' na terre des hommes yanawasilisha ripoti yao ya 24 inayojulikana kama "ukweli kuhusiana na sera za maendeleo" katika mkutano mjini Berlin (08.09.2016).

DW Global 3000 Millenniums-Dorf Sauri
Kijiji cha milenia magharibi mwa KenyaPicha: DW

Bila shaka unakumbuka msikilizaji neno hili "Malengo ya maendeleo ya milenia". Ni neno kutoka Umoja wa Mataifa kwa matarajio ya kupunguza umasikini duniani kwa nusu ifikapo mwaka 2015. Neno hilo limetumika na kufahamika kwa lengo la kupambana na njaa. Malengo haya yana nia ya kuongeza kipato , elimu na kupunguza vifo vya watoto na akina mama wakati wa kujifungua. Pia ni kuhusu haki na demokrasia.

Mchoro wa msaada wa maendeleo kwa Ujerumani katika mwaka 2015

Ripoti ya Marcel Fürstenau kuhusiana na ripoti ya 24 ya mashirika ya kutoa misaada ya Welthungerhilfe na terre des hommes itakayowasilishwa leo mjini Berlin huyu hapa Sekione Kitojo.

Pamoja na hamasa kubwa katika malengo hayo, hata hivyo ni sehemu tu ya malengo hayo yaliyofikiwa. Kwa mujibu wa shirika la chakula la Umoja wa mataifa FAO mwishoni mwa mwaka jana, karibu watu milioni 795 walikuwa bado na matatizo ya njaa, baada ya watu bilioni moja kuwa wanakabiliwa na njaa katika mwaka 1990. inasomwa humu studioni na Sekione Kitojo.

Kutoka , Malengo ya maendeleo ya milenia , MDG kama yanavyojulikana , baada ya mkutano wa Umoja wa mataifa mjini New York , maneno hayo yalibadilishwa na kuwa Malengo ya maendeleo endelevu, yaani SDG.

Mchoro wa msaada wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa mataifa WFP

Tofauti na malengo ya milenia

Maendeleo haya endelevu yanatarajiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2030. Tofauti kubwa kati ya MDG na SDG ni kwamba , malengo hayo si tu kwa watu masikini na mataifa masikini pekee duniani.

Hata Ujerumani ni nchi inayoendelea ,ambapo inalazimika kutoza kodi katika masuala ya matumizi ya chakula, uzalishaji na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi. Na hali hiyo inazungumziwa leo Jumatano (07.09.2016) katika mkutano wa asasi za Welthungerhilfe na terre des hommes mjini Berlin.

Waziri wa wizara ya maendeleo na ushirikiano wa kimataifa nchini Ujerumani Gerd MuellerPicha: Bernd Riegert

Sera za maendeleo

Ni ripoti ya 24 ya mashirika hayo ya kutoa misaada ikiwa na kauli mbiu "hali halisi ya sera za maendeleo". Pamoja na hayo alama nzuri mara hii hakuna. Lakini hali jumla haionekani kuwa mbaya, kama inavyoonekana.

Wizara ya maendeleo ya uchumi na ushirikiano BMZ imesifiwa kwa dhamira yake , na kutumia ukikosoa na mapendekezo kwa ajili ya kufanya vizuri zaidi.

Akina mama na watoto nchini Sudan kusini ambao wanahitaji msaada wa maendeleoPicha: DW / F. Abreu

Kwa mfano ni juhudi maalum , zijulikanazo kama "dunia bila njaa". Katika hilo, waziri wa wizara hiyo Gerd Mueller ameyataka mataifa yale ambayo yamepiga hatua ndogo za maendeleo duniani kuchukua juhudi zaidi.

Hadi sasa zipo bado euro bilioni 1.4 kwa ajili ya mipango hiyo kutoka mwaka 2015 kwa mujibu wa wizara hiyo. Kiasi kama hicho cha fedha kitapatikana pia mwaka huu.

Sifa hizo za mashirika ya kutoa misaada hata hivyo zinafuatia ukosoaji mkubwa. Mipango inafanywa kwa haraka haraka ikiwa ndio msingi wa tatizo katika tathmini kuhusiana na njaa na utapia mlo kwasababu mashirika yasiyo ya kiserikali katika mataifa hayo hayahusishwi ama yanashirikishwa kwa kiasi kidogo tu. Hii ina maana kuna nia njema, lakini bila ya kuchunguzwa kwa undani.

Mwandishi : Fürstenau, Marcel / Sekione Kitojo

Mhariri: Caro Robi