MISAADA YA KIUTU KUIMARISHWA:
31 Desemba 2003TEHRAN: Inakhofiwa kuwa hadi watu 50,000 wamefariki katika mtetemeko wa ardhi uliotokea siku ya Ijumaa katika mji wa Bam nchini Iran.Huenda ikawa elfu kadhaa ya watu bado wamo chini ya majengo yalioteketea.Maafisa wamesema hayo ni maafa makubwa kabisa kupata kutokea katika miaka ya hivi karibuni.Hadi hivi sasa kiasi ya maiti 30,000 zimeshazikwa.Siku nne baada ya mtetemeko,wasaidizi waliweza kumuokoa mwanamke mmoja aliekuwa mjaa mzito.Kwa jumla watu 3,000 waliweza kuokolewa chini ya nyumba zilizoporomoka.Kuanzia jumatano mabuldoza yataanza kuondosha mabakio ya majengo yalioteketea.Tume za kimataifa za uokozi,ikiwa ni pamoja na wataalamu 50 wa Kijerumani zimesharejea nyumbani.Sasa misaada ya kiutu kwa ajili ya kiasi ya watu 100,000 wasiokuwa na mahala pa kuishi,imeimarishwa katika eneo hilo la mtetemeko.