1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Misaada yapelekwa kwenye Wakurdi wengi Syria

25 Januari 2026

Misaada ya kiutu imepelekwa katika mji wenye idadi kubwa ya Wakurdi wa Kobane Kaskazini mwa Syria. Mamlaka zimesema msafara huo wa malori 24 ya misaada umeratibiwa na serikali na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa.

Misaada ya kiutuimepelekwa katika eneo lenye watu wengi wa jamii ya Wakurdi la Kobane
Malori ya yakiwa katika msafara kupeleka misaada katika eneo lenye uhitaji SyriaPicha: Omar Sanadiki/AP/picture alliance

Hayo yanajiri muda mfupi baada ya jeshi nchini humo kutangaza kurefushwa kwa muda wa makubaliano ya kusitisha vita  kati yake na vikosi vinavyoongozwa na wapiganaji wa Kikurdi (SDF).

Wanaharakati wapaza sauti kuhusu hali mbaya ya kiutu

Wanaharakati wamekuwa wakionya kuwa hali ya kiutu ni mbaya katika mji huo wenye ghasia ulio mpakani na uturuki. Hali hiyo imetokana na mapigano ya hivi karibuni kati ya vikosi vyenye uhusiano na serikali ya Syria dhidi ya wanamgambo wa SDF.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW