Misaada zaidi kupambana na magonjwa
28 Septemba 2007Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na nchi 30 fadhili siku ya Alkhamisi katika mkutano wa Berlin.Ujerumani itachangia Euro milioni 600 hadi mwaka 2010.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan,kama mwenyekiti wa mkutano wa mjini Berlin, amesifu mchango wa wafadhili.Amesema,malengo yaliyowekwa na jumuiya ya kimataifa ni hatua muhimu katika jitahada za kupambana na magonjwa duniani.
Hapo awali,Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,akiwa mwenyekiti wa sasa wa Kundi la Mataifa Manane Tajiri duniani- G8,alitoa wito wa kuwepo uratibu bora zaidi wa mipango ya afya.
Mfuko wa Dunia uliozinduliwa mwaka 2002 kwa jitahada za Kofi Annan,hadi hivi sasa umefanikiwa kuokoa maisha ya watu wapatao milioni 2.