Misako na kamatakamata ya ufisadi yaendelea Ukraine
12 Novemba 2025
Matangazo
Wizara ya sheria ya nchi hiyo iliyo kwenye vita na Urusi, ambayo kwa sasa inaongozwa na Galushchenko imethibitisha kufanyika uchunguzi huo, na kwamba mwanasiasa huyo amekubali kutoa ushirikiano kwa mamlaka za upelelezi.
Baadaye, Ofisi ya Kupambana na Ufisadi ya Ukraine (NABU) ilitowa notisi ya tuhuma dhidi ya naibu waziri mkuu wa zamani, Oleksiy Chernyshov, ambaye amekuwa akichunguzwa tangu mwezi Juni kwenye kesi nyengine inayohusiana na sekta ya ujenzi.
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, Serhiy Savytsky, amethibitisha notisi hiyo.
Licha ya kukabiliwa na uvamizi wa Urusi kwa miaka minne sasa, serikali ya Ukraine inayoongozwa na Rais Volodymyr Zelensky imekuwa ikishutumiwa kwa kuendekeza ufisadi.