1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mishahara ya wakuu Rwanda kuwasaidia raia

6 Aprili 2020

Mishahara ya wanasiasa na wafanyakazi wakuu wa umma nchini Rwanda mwezi huu itaelekezwa katika mipango ya misaada kuwasaidia maskini kupambana na athari za virusi vya corona.

Präsident Ruanda Paul Kagame
Picha: Imago/Zumapress/E. Contini

Kulingana na Waziri mkuu Edouard Ngirente jambo hilo litaonyesha mshikamano na raia ambao wamekuwa katika kipindi kigumu kutokana na marufuku ya kutotoka nje kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Serikali imekuwa ikitoa chakula kwa karibu wakaazi 20,000 wasiojiweza kiuchumi katika mji mkuu Kigali ingawa ni wengi wanaohitaji msaada huo katika nchi yenye idadi ya watu milioni 12 ambapo thuluthi moja wanaishi katika umasikini.

Haijabainika wazi lakini serikali itapata kiasi gani cha fedha kutokana na mishahara hiyo ya maafisa wakuu serikalini. Rwanda iliweka marufuku ya kutotoka nje kuanzia Machi ishirini na moja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW