1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufunguzi wa kivuko cha Rafah kujadiliwa mjini Cairo

1 Juni 2024

Maafisa wa Misri watakutana na wenzao wa Israel na Marekani kesho Jumapili kujadili hatua za kukifungua tena kivuko cha Rafah, ambacho ni muhimu katika kupitisha misaada kuelekea eneo lililozingirwa la Ukanda wa Gaza.

Rafah
Kivuko cha Rafah kilifungwa tangu Israel ilipokamata eneo hilo la Palestina mwezi Mei Picha: Mohammed Abed/AFP/Getty Images

Televisheni ya Al Qahera nchini Misri iliyo na mawasiliano na maafisa wa kijasusi wa taifa hilo la kiafrika, ilimnukuu afisa mmoja ambaye haikumtaja jina, akisema Cairo inataka wanajeshi wote wa Israel waondoke kati ya mpaka wa kusini mwa Gaza na Misri.

Kivuko hicho kilifungwa tangu Israel ilipokamata eneo hilo la Palestina mwezi Mei hatua ambayo imepunguza utaratibu wa mtiririko wa msaada katika eneo hilo linalokumbwa na vita.

Vita vya Gaza: Blinken akutana na Netanyahu

Tangu wakati huo Misri na Israel zimekuwa zikilaumiana kuzuwia msaada kuingia Gaza kupitia Rafah. 

Mamlaka za Misri zimekataa kushirikiana na Israel ikiona ni bora kushirikiana na mashirika ya kimataifa au wapalestina wenyewe. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW