1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri na India zasaini mikataba ya kuimarisha mahusiano

26 Juni 2023

Waziri mkuu wa India Narendra Modi Jumapili alipata makaribisho ya heshima kubwa nchini Misri alikopokelewa na rais AbdelFatah El-Sissi katika ikulu ya mjini Cairo.

Ägypten Kairo |  Abdel Fattah al-Sisi und Narendra Modi
Picha: Egyptian Presidency Media Office/AP/picture alliance

Viongozi hao wawili walisaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao na kuwa  kile kilichoitwa ushirikiano wa kimkakati, ikimaanisha nchi hizo zimeridhia kuongeza ushirikiano na kuwa na mikutano ya mara kwa mara, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa.

Soma pia: India yaiombea Afrika uanachama wa kudumu, G20

Modi ni waziri mkuu wa kwanza  wa India kufanya ziara ya kiserikali nchini Misri katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili. Aliwasili Jumamosi mjini Cairo na ziara hiyo ya siku mbili imekuja miezi sita baada ya rais El Sisi kuitembelea India akiwa kama mgeni rasmi wa heshima katika siku ya kumbukumbu ya  Uhuru wa India.

Serikali hizo mbili pia zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta za kilimo, utafiti wa masuala ya akiolojia, vitu vya kale na sheria.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW