1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Misri na Saudia kuimarisha ushirikiano

3 Aprili 2023

Viongozi wa Misri na Saudi Arabia wamekutana nchini Saudia katika ziara ya kwanza ya viongozi wakuu katika miezi kadhaa wakati Misri inapambana na mzozo wa kiuchumi wa ndani.

DW Middle East - Saudi Arabia: National makeover in full swing
Picha: ATHIT PERAWONGMETHA/AFP/Getty Images

Rais wa Misri Abdel Fatah El Sissiamefanya mazungumzo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman jana usiku na kujadili masuala ya ushirikiano wakati nchi hizo mbili zikiwa kwenye mvutano uliodumu kwa miezi kadhaa.

SOMA PIA; Misri na Iraq zazidi kuimarisha mahusiano yao

Katika taarifa msemaji wa rais wa Misri Ahmed Fahmy, amesema kwamba viongozi hao walizungumzia kile alichokitaja kama "umuhimu wa kuunga mkono ushirikiano wa pamoja katika nyanja zote." na wamekubaliana kuendelea na hatua za uratibu na mashauriano kuhusu ajenda za kikanda na kimataifa.

Hata hivyo taarifa hiyo haikutoa maelezo zaidi. Ziara hiyo ya kushtukiza ilikuwa ya kwanza kutangazwa ya mkutano kati ya viongozi hao tangu walipokutana nchini Qatar wakati wa ufunguzi wa Kombe la Dunia. El-Sissi pia alimpokea bin Salman huko Cairo mnamo Juni 2022 kabla ya ziara ya Rais Joe Biden Mashariki ya Kati.

Mzozo wa kiuchumi ukoje?

Picha: John Macdougall/AP Photo/picture alliance

Mkutano huo unajiri wakati serikali ya Sissi inajitahidi kushinda mzozo wa kiuchumi unaohusishwa na vita barani Ulaya, lakini wakosoaji wanasema umekutokana na usimamizi mbaya wa uchumi.

Misri na Saudia pia wanalenga kurekebisha uhusiano wao uliovunjika na mataifa mengine ya kikanda, kama vile Iran na Uturuki.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudia, Maafisa wengine kutoka nchi zote mbili walihudhuria mazungumzo hayo, wakiwemo Abbas Kamel, Mkuu wa Mamlaka ya Ujasusi ya Misri, na Musaed bin Mohammed Al-Aiban, mshauri wa usalama wa taifa wa Saudia.

SOMA PIA; Misri imeahidi "mshikamano na huruma" kwa Syria

Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Kiarabu yamekuwa wasambazaji wakuu wa misaada kwa serikali ya Misri, ambayo imekuwa ikijitahidi kuondokana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Mnamo 2022, Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu uliahidi jumla ya dola bilioni 22 kama amana na uwekezaji wa moja kwa moja nchini Misri, kwa nia ya kuimarisha uchumi uliozorota baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Malumbano ya mtandaoni kati ya watu mashuhuri katika nchi hizo mbili yaliibuka baada ya kuchapishwa kwa maoni katika gazeti la serikali ya Misri mwezi Februari, likisema kwamba Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba hayakuwa na haki ya kukosoa jinsi serikali ya Misri inavyoshughulikia uchumi wake.

Lakini rais el-Sissi alizima malumbano hayo alipozungumza katika Mkutano wa kimataifa wa Serikali huko Dubai mwezi Februari, na kusifu falme za Ghuba kwa kuisadia na misaada wa kifedha katika miaka iliyopita.

 

/AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW