SiasaMisri
Misri na Uturuki zakubaliana kuboresha uhusiano
30 Mei 2023![WM in Katar 2022 | Treffen Recep Tayyip Erdogan und Abdulfettah al-Sisi](https://static.dw.com/image/63827527_800.webp)
Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa ofisi ya rais wa Misri, Rais Abdel-Fattah al-Sissi alimpigia simu mwenziwe Recep Tayyip Erdogan na kumpongeza kuchaguliwa tena kuwa rais wa Uturuki.
Soma pia: Misri imeahidi "mshikamano na huruma" kwa Syria
Uhusiano kati ya Misri na Uturuki ulidorora katikati ya mwaka 2013 baada ya jeshi likiongozwa na al-Sissi, kumpindua rais wa Misri kwa wakati huo Mohammed Morsi.