1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoMisri

Misri yamfuta kazi kocha wa timu ya taifa ya kandanda

5 Februari 2024

Misri imetangaza kumfuta kazi kocha wa timu ya taifa ya kandanda Rui Vitoria pamoja na jopo lake la kiufundi kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo katika michuano ya mataifa ya Afrika AFCON inayoendelea Ivory Coast.

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Misri Rui Vitoria
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Misri Rui Vitoria akizungumza na waandishi wa habari mjini AbijanPicha: Braima Darame/DW

Kocha huyo raia wa Ureno ametimuliwa baada ya timu ya Misri  ambayo imetwaa kombe la Afrika mara saba, kushindwa kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Siku ya Jumatano Februari 7,2024 ni hatua ya nusu fainali ambapo Nigeria watachuana na Afrika Kusini na baadaye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakimenyana na wenyeji Ivory Coast.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW