1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

el-Sissi apendekeza kusitishwa mapigano Ukanda wa Gaza

28 Oktoba 2024

Rais wa Misri AbdelFatah el-Sissi amesema nchi yake imependekeza siku mbili za usitishaji mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas, ambapo katika muda huo mateka wanne wanaozuiliwa Gaza wataachiliwa huru.

Waziri Mkuu wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi hivi karibuni alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken katika hatua za kusaka suluhu ya amaniPicha: Egyptian President Office/APAimages/IMAGO

Rais El-Sissi amesema pendekezo hilo linajumuisha pia hatua ya kuachiwa huru baadhi ya wafungwa wa Kipalestina pamoja na kupelekwa msaada wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Hata hivyo, sio Israel wala kundi la Hamas waliotowa tamko lolote hadi sasa kuhusiana na mapendekezo hayo, wakati duru mpya ya mazungumzo ikitarajiwa kufanyika nchini Qatar.

Mkuu wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad, alikwenda Doha jana Jumapili kwa ajili ya mazungumzo na waziri mkuu wa Qatar pamoja na mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA ikiwa ni juhudi za kumaliza vita na kupunguza mivutano ya kikanda iliyoongezeka.