1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yasema haitakubalia mabadiliko kwenye mpaka Gaza

18 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Badr Abdelatty, amesema nchi hiyo haitokubali mabadiliko yoyote katika utaratibu wa usalama wa mpaka wake na Gaza uliokuwepo kabla ya vita vya Israel na Hamas.

Misri | Antony Blinken mjini Kairo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na mwenzake wa Misri Badr Abdelatty mjini Cairo, Septemba 18, 2024.Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Badr Abdelatty, amesema nchi hiyo haitokubali mabadiliko yoyote katika utaratibu wa usalama wa mpaka wake na Gaza kabla ya vita kuanza kati ya Israel na Hamas mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Usalama wa mpakani na iwapo Israel itaendelea kuwabakiza wanajeshi wake kilomita 14 katika eneo lisolokuwa na vita la kivuko cha Philadelphi, imekuwa suala muhimu katika mazungumzo ya kutafuta makubaliano ya kusitisha mgogoro wa Mashariki ya kati na kuwaachia mateka wa Israel wanaoendelea kuzuiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas.

Soma pia: Blinken awasili Cairo kuendeleza juhudi za amani Mashariki ya kati

Wanajeshi wa Israel waliingia katika kivuko cha Philadelphi mwezi Mei walipokuwa wanaendeleza operesheni yao ya kijeshi katika mji wa Rafah.

Misri ambayo ni mmoja ya wapatanishi katika mgogoro huo imesema Israel ni lazima iwaoandoe wanajeshi wake na uwepo wa wapalestina ni lazima urejeshwe katika kivuko cha Rafah kati ya rasi ya Sinai na Gaza.