1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yasema haitokubali vikosi vya Israel kwenye mpaka wake

26 Agosti 2024

Misri imesema haitakubalina na hatua ya vikosi vya Israel kuendelea kuwepo kwenye mpaka wake na Ukanda wa Gaza, vyombo vya habari vyenye uhusiano na serikali vimeripoti hii leo.

Israel | Rafah| Gaza
Vikosi vya Israel kwenye mpaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza.Picha: Gil Cohen Magen/Xinhua/picture alliance

Cairo, ambayo ni miongoni mwa wapatanishi wakuu katika juhudi za kupatikana kwa makubaliano kati ya Hamas na Israel kuelekea vita vya Gaza, imeziambia pande zote kwamba haitakubali uwepo wa aina yoyote wa jeshi la Israel katika ukanda wa kimkakati wa Philadelphi, shirika la habari la Al-Qahera lenye uhusiano na serikali limesema likinuu duru za ngazi za juu.

Hoja ya msingi katika mazungumzo ya kusitisha mapigano imekuwa ni wito kwa Israel kuondoa vikosi vyake katika eneo hilo, pamoja na kivuko cha Rafah, ambacho ni pekee kutoka ardhi ya Palestina ambacho hakikudhibitiwa moja kwa moja na Israel.

Vikosi vya Israel viliukamata upande wa Palestina ulioko Rafah mapema mwezi Mei, na kufunga njia muhimu ya kupitisha misaada, hatua iliyokosolewa mara kadhaa na Misri na mataifa mengine.