Misri yawasilisha juhudi kumaliza mzozo Libya
6 Juni 2020Kiongozi huyo wa Misri amewasilisha juhudi hiyo mjini Cairo akiwa pamoja na kamanda Khalifa Haftar, mkuu wa jeshi linalojiita jeshi la taifa la Libya.
Pendekezo hilo la juhudi linatoa wito wa kuondoka kwa wanamgambo wa kigeni kutoka Libya, ikiwa na maana ya wapignaji mamluki wanaodaiwa kuingizwa nchini humo na Uturuki wakisaidia mahasimu wa Haftar.
Wanajeshi watiifu kwa Haftar wamepata wamepata hasara kubwa kijeshi dhidi ya majeshi yenye mafungamano na serikali ya makubaliano ya kitaifa GNA inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa na yenye makao yake mjini Tripoli.
Rais Abdel-Fattah el-Sissi alitangaza juhudi hizo katika sherehe mjini Cairo iliyohudhuriwa na kamanda Haftar pamoja na Aguila Saleh , spika wa baraza la wawakilishi linalofanya shughuli zake Tobruk. El-Sissi amesema juhudi hizo, ambazo zinajumuisha kusitisha mapigano , zina lenga ksafisha njia kwa ajili ya uchaguzi katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.
Hakuna maelezo ya mara moja kutoka katika serikali inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa katika mji mkuu Tripoli.
Jeshi la Haftar
Jeshi la Haftar linalojulikana kama Libyan Arab Armed Forces lililoko upande wa mashariki lilianzisha mashambulizi mwaka ulipita kuukamata mji mkuu Tripoli. Lakini hivi karibuni amepoteza maeneo muhimu ya kimkakati magharibi mwa Libya baada ya Uturuki kuongeza msaada wake kwa makundi kadhaa ya wanamgambo ambayo yanamafungamano na serikali yenye makao yake makuu mjini Tripoli.
Majeshi ya Haftar yanaungwa mkono na Ufaransa, Urusi, Jordan , Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na washirika wengine muhimu katika mataifa ya Kiarabu.
Pamoja na Uturuki, serikali mjini Tripoli inaungwa mkono na italia na Qatar. Libya imekuwa katika machafuko tangu mwaka 2011 wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe viliposababishwa kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mrefu Moammar Gaddafi, ambaye baadaye aliuwawa.
Nchi hiyo imegawanyika katika serikali hasimu upande wa mashariki na magharibi, kila moja ikiungwa mkono na makundi yenye silaha pamoja na serikali za kigeni.