MISSISSIPPI:Kumbunga Katrina chaua watatu nchini Marekani
30 Agosti 2005Kimbunga kikali Katrina kimeshaua watu watatu na kusababisha hasara kubwa katika jimbo la Mississippi kusini mwa Marekani.
Mvua kubwa na upepo mkali umesababisha kufungwa kwa viwanja vya ndege na ukosefu wa nishati ya umeme katika maalfu ya nyumba.
Licha ya kupungua nguvu kidogo, watu wanaofanya juhudi za kuwaokoa waathirika wanashindwa kufika katika sehemu ambazo hasa zimekumbwa na kimbunga hicho.
Jimbo la Louisiana jana lilikumbwa na dhoruba kali ya pepo zilizofikia kasi ya kilometa 240 kwa saa.
Maalfu ya watu wamehamishwa katika mji wa New Orleans kutokana na nyumba zao kufunikwa na maji hadi kwenye mapaa.
Kimbunga Katrina pia kimesababisha bei ya mafuta kupanda na kuvuka dola 70 kwa pipa kufuatia kuhamishwa kwa majukwaa ya kuzalishia mafuta kwenye ghuba ya Mexico.
.