1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mito kuimarisha sheria za ulinzi wa data

5 Mei 2009

Mtandao wa Intanet,barua pepe na simu za mkono ni njia za kuwasiliana bila ya kuwepo mipaka lakini huwezesha pia upelelezi usio na kikomo.

Bundesinnenminister Wolfgang Schäuble (CDU) beantwortet am Donnerstag (04.09.2008) in Berlin Fragen der Medienvertreter. Die Bürger sollen künftig einer Weitergabe ihrer Personen-Daten ausdrücklich zustimmen müssen. Ein entsprechendes Gesetz solle bis Ende November im Kabinett beschlussfähig sein, sagte Schäuble nach einem Spitzentreffen von Bund und Ländern zum Datenschutz in der Bundeshauptstadt. Foto: Rainer Jensen dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble.Picha: picture-alliance/ dpa

Watetezi wa hifadhi ya data wanapaza sauti na kudai kuwa hali hiyo inapaswa kuzuiliwa kisheria.Na leo katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin, kunafanywa mkutano wa siku mbili kuhusu hifadhi ya data. Lakini mkutano huo unaowaleta pamoja wataalamu wa masuala ya kisiasa, uongozi na uchumi unafanywa chini ya kivuli cha mlolongo wa kashfa za hifadhi ya data zilizotokea katika miezi iliyopita.Makampuni kama Telekom,Deutsche Bahn au maduka makubwa ya vyakula -yote kwa kiwango fulani yalihusika na vitendo vya kuwapeleleza wafanyakazi wake kinyume na sheria. Sauti zilipazwa kutaka ulinzi bora zaidi hasa kuhusu wafanyakazi - na miswada ya sheria imewasilishwa, lakini hadi sasa hakuna hatua timamu iliyochukuliwa.

Kwa mfano,mwezi wa Desemba mwaka uliopita,Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble aliwasilisha mswada wa sheria ambao hasa ulihusika na kashfa ya biashara ya anuani za makampuni ya binafsi. Chanzo ni kuuzwa kwa data binafsi za mamilioni ya wateja, kwa makampuni yanayotaka kandarasi mpya. Miongoni mwa data zilizotolewa ni zile zilizohusika na akaunti za wateja hao.

Wapinzani wa mtindo huo ulio halali, wanasema kuwa biashara ya aina hiyo iruhusiwe tu ikiwa idhini imetolewa na yule anaehusika na data hizo. Mwito huo umeungwa mkono na waziri wa ndani Schäuble.Yeye akaongezea kuwa kila kisa lakini kizingatiwe peke yake kuamua vipi data za wafanyakazi zitakavyotumiwa ndani ya kampuni yenyewe.

Mkosoaji mkubwa kabisa wa sheria za hivi sasa kuhusu hifadhi ya data ni Gisela Piltz wa chama cha kiliberali cha FDP. Bungeni,mwanasiasa huyo tangu miaka na miaka, anagombea sheria kali zaidi bila ya kufanikiwa. Kwa upande mwingine, Alexander Dix anaehusika na ulinzi wa data mjini Berlin anasema si sheria bora zaidi tu inayohitajiwa kwa dharura.Yeye anataka fidia ilipwe kwa wahanga wa kashfa zinazohusika na hifadhi ya data.

Lakini kwa kipindi cha hivi sasa hakuna matarajio ya kufanywa marekebisho kuhusu sheria ya hifadhi ya data,kwani baada ya miezi miwili bunge litakuwa katika mapumziko ya majira ya joto na uchaguzi mkuu unafanywa mwezi wa Septemba. Kwa hivyo,kuna hofu kuwa suala la ulinzi wa data litaendelea hivyo hivyo kama ilivyo baada ya kila kashfa: Mada hiyo inasahauliwa mpaka kashfa nyingine inapoibuka.

Mwandishi: M.Fürstenau/ P.Martin

Mhariri: Miraji Othman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW