1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mitsotakis awasili Israel kuonesha mshikamano

23 Oktoba 2023

Waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis amewasili mjini Jerusalem mapema hii leo kukutana na mwenzake wa Israel Benjamin Netanyahu.

Waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis
Waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos MitsotakisPicha: Dimtiris Papamitsos/Greek Prime Minister's Office/AP/dpa/picture alliance

Mitsotakis amefika Jerusalem wakati vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas vikizidi kushika kasi, huku kukiripotiwa vifo vya Wapalestina 5,000 hadi sasa.

Netanyahu amemshukuru Mitsotakis kwa kuonyesha mshikamano, sambamba na serikali na watu wa Ugiriki.   

soma pia:

Mitsotakis amesema tangu mwanzo Ugiriki iliunga mkono haki ya Israel kujilinda kwa kuzingatia sheria ya kimataifa, na kuweka tofauti ya wazi kabisa kati ya Hamas na Wapalestina, huku ikiahidi kuendelea kuisaidia.

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza imesema watu zaidi ya 5,000 wameuawa katika Ukanda huo uliozingirwa, tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi wiki mbili zilizopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW